Sunday, 25 November 2018

MSHAMBULIAJI WA SIMBA SC SALAMBA ASAKWA NA WAZUNGU;




Timu tatu kutoka barani Ulaya zimeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Simba, Adam Salamba tayari zimepewa 'makabrashi' ya takwimu ya mchezaji huyo kwa ajili ya kwenda kuyafanyia kazi.

Meneja wa Salamba, Jamal Kisongo amesema kuwa hadi sasa kuna timu tatu ambazo zimeleta ofa ya kumtaka mteja wake.

"Timu 3 zimeleta ofa kumtaka Salamba akafanye majaribio ulaya, walihitaji takwimu zake kujua amecheza mechi ngapi msimu uliopita na msimu huu na mabao aliyofunga, tayari tumekamilisha zoezi hilo kwa kuwasilisha video zake zote," alisema.

Salamba amefunga mabao 2 mpaka sasa kwenye Ligi Kuu akiwa ndani ya kikosi cha Simba alisajiliwa akitokea timu ya Lipuli.

No comments:

Post a Comment

Tex post